MBUNGE RITHA KABATI AZISAIDIA SHULE MADAWATI
Viongozi mbalimbali wa Manispaa ya Iringa wakitazama msaada wa madawati ambao wamepatiwa na mbunge Ritha Kabari.
Mbunge Ritha Kabati (Viti maalumu CCM) mkoa wa Iringa akiweka saini ya kupokea madawati 100 kutoka kwa mwakirishi wa mkurugenzi wa bodi ya michezo ya kubahatisha, makabidhiano yaliyofanyika katika uwanja wa Sabasaba mjini Iringa.
Mwakirishi wa mkurugenzi mkuu wa bodi ya michezo ya kubahatisha (Gaming Board Of Tanzania) Sadick Soud Kasuhya akiweka sahihi ya kukabidhi madawati 100 kwa mbunge Ritha Kabati.
Wakipeana pongezi ya kufanikisha mpango
wa kuikabiri changamoto ya uhaba wa madawati Manispaa ya Iringa, baada
ya kukabidhi madawati 100 kwa idara ya elimu manispaa ya Iringa kwa
lengo la kupunguza tatizo la wanafunzi kukaa Sakafuni.
Akikabidhi madawati hayo kwa idara ya elimu Manispaa ya Iringa, Kabati amesema hatua hiyo imekuja baada ya kutambua uwepo wa tatizo hilo kwa shule za Iringa na hivyo kuona umuhimu wa kuwatafuta wahisani ili kusaidiana kutatua tatizo hilo, ambalo linachangia hata elimu mkoani humo kudumaa.
Kabati amesema baada ya kutambua uwepo wa changamoto kubwa ya madawati kwa shule nyingi mkoani Iringa, aliwatafuta wadau na wahisani mbalimbali ili kusaidia kuikabilia changamoto hiyo.
Amesema jambo hilo amejifunza pindi alipokuwa akialikwa kuhudhuria mahafali ya shule hizo ambapo baadhi ya wanafunzi hata kwa shule za manispaa walikuwa wakikosa madawati na kupelekea kukaa chini.
"Nilipoona ukubwa wa tatizo la madawati niliwatafuta wahisani na wadau, nikawaandikia barua nikiwaomba wanisaidie, ninashukuru Gaming Board Of Tanzania, bodi ya michezo ya kubahatisha wamenisaidia tena kwa kiwango kile kile nilichokuwa nimekiomba, ninawashukuru sana," Alisema Kabati.
Naye ofisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Sadick Kasuhya ambaye ni muhisani wa msaada huo, amesema madawati hayo yamegharimu jumla ya shilingi Milioni 6 na laki 5,huku wakijipanga zaidi kusaidia sekta hiyo nyeti ya elimu.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Iringa Abeid Kiponza amesema kuna haja kwa wabunge wengine wakaiga mfano wa kiongozi huyo ili kuwaepusha wanafunzi na adha ya kukaa sakafuni.
Kiponza amesema mkoa wa Iringa hauna sababu ya shule wanafunzi wake wakakosa madawati kutokana na kuwepo kwa mashamba makuybwa ya Miti ikiwa pamoja na Msitu wa taifa wa Sao hill.
"Kwanza wabunge wengine mkoani Iringa waige mfano huu, wakifanya jambo kama hili tatizo la uhaba wa madawati kamwe halitakuwepo kwa shule zetu zote mkoani Iringa, hii ni aibu sana, tuna msitu ule wa Sao hill, lakini na sie eti tunaingia kwenye kati ya mikoa yenye tatizo la madawati, hii ni aibu sana, huyu mbunge niwa viti maalumu, n\hana mfuko wa jimbo, lakini amekuwa akifanya mambo makubwa sana, ni msaada wetu mkubwa, licha ya kuwa CCM jimbo la Iringa hatuna mbunge lakini Ritha Kabati huyu anatuwakirisha vyema, " alisema.
Hata hivyo ofisa elimu vifaa na takwimu Manispaa ya Iringa Jane Mwalongo amesema Manispaa ya Iringa bado ina upungufu wa madawati zaidi ya elfu 6, kutokana na kuwa na wanafunzi 26, 858, huku idadi ya madawati ikiwa ni 7415 pekee.
Aidha Mwalongo amesema tatizo la uhaba wa madawati linachangia kupunguza kiwango cha uelewa kwa wanafunzi katika masomo, na kuwa Manispaa inauhitaji wa madawati zaidi ya elfu 13,429, n hiyo ni kutokana na kuwa na upungufu wa madawati 6014.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni