BODABODA WAMSURUBISHA ASKARI MBELE YA KAMANDA, NAO ABIRIA WASIO VAA HELMENT SASA KUONJA JOTO YA JIWE
Dereva wa Bodaboda akipokea cheti cha uhitimu wa mafunzo ya uendeshaji salama wa Pikipiki, katika ukumbi wa Orofea Kitanzini katika manispaa ya Iringa, hafla iliyohudhuliwa pia na mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Iringa Bw. Salm Abri- Asas.
Cheti ambacho wamekabidhiwa madereva wa Bodaboda manispaa ya Iringa baada ya kuhitimu mafunzo hayo, yenye lengo la kupunguza (kutokomeza) ajali za barabarani, kwa kutoa elimu sahihi ya namna ya udereva huo na ishara za barabarani.
Mkaguzi wa vyombo vya moto (Vehicle Inspector) SP Steven Nyandongo, akiongoza madereva kula kiapo cha udereva wa kujihami, katika hafla ya kukabidhiwa vyeti wahitimu hao.
"Nitaheshimu sheria na kanuni za usalama barabarani siku zote za maisha yangu, nitaendesha Pikipiki yangu kwa mwendo unaotakiwa, sitaacha kuvaa kofia ngumu mimi na abiria wangu wakati wote niendeshapo Pikipiki, Sitakubali kupakia abiria zaidi ya mmoja katika Pikipiki yangu, nitaheshimu ishara na alama zote za barabara," Wakisema.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama barabarani Bw. Salim Abri- Asas, akizungumza na wahitimu wa kozi ya udereva Pikipiki, ambapo ametoa fulsa kwa madereva 100 wasio na uwezo wa kugharamia kozi, kwa kuwalipia ada ya mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa chama cha waendesha Pikipiki (Bodaboda) Joseph Mwambobe, akisoma lisara ya wanachama wake mbele ya uongozi wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa, idara ya biashara manispaa pamoja na kamati ya usalama barabarani, katika hafla hiyo.
SP Zakaria Benard- Mratibu wa Bodaboda Mkoa wa Iringa.
Kamanda ACP Athmani Mungi ( wa kwanza kushoto) akiwa na mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Bw. Salm Abri- Asas, wakisikiliza maelezo ya wahitimu hao.
SP- Zakaria Benard- Mratibu wa bodaboda mkoa wa Iringa akitoa taarifa ya mafunzo hayo ya madereva zaidi ya 130 waliopatiwa elimu ya udereva sahihi.
Mwalimu wa mafunzo ya udereva (wa kwanza kulia) akiwa na mwenyekiti wa chama cha waendesha Bodaboda, ambaye anaandika kumbukumbu za kikao hicho.
SP- Msangi- mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Iringa, akiwa na Vehicle Inspector Steven Nyandongo katika hafla hiyo.
Maafande wa kitengo cha usalama barabarani wakisikiliza kwa umakini taarifa ya chama cha waendesha bodaboda.
Madereva wakifurahia jambo.
Wahitimu wa mafunzo ya udereva wa bodaboda, wakifuatilia jambo katika hafla hiyo.
Hayo yalizunbgumzwa na kamnada wa jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ASP Athman Mungi wakati wa hafla ya kukabidhi vyeti vya kufuzu mafunzo ya waendesha Pikipiki 140 wa Manispaa ya Iringa, katika ukumbi wa Orofea Mjini Iringa.
ASP Mungi amesema kamwe jeshi hilo halitawavumilia abiria wa aina hiyo kutokana na ukweli kuwa pindi inapotokea ajlai wanaopata madhara ni madereva pamoja na abiria hao, na kuwa hakuna sababu ya kumtoza faini dereva aliyempakia abiria mvunja sheria.
"Sioni kama kunasababu ya kuwapiga faini au kuwapa adhabu madereva wakati abiria ndiyo mwenye makosa, kuanzia sasa tukimkuta abiria ambaye hajavaa Elment ajue yeye ndiyo mwenye kuubeba msalaba wa adhabu ya uvunjaji wa sheria hiyo, na siyo dereva, tunataka kuhakikisha ajali zitokanazo na Pikipiki zinapungua au kuisha akabisa," Alisema Mungi.
Aidha Mungi aliwataka wanasiasa, viongozi wa dini na wananchi kwa ujumla kushirikia katika udhibiti wa vitendo viovu vinavyofanya na baadhi ya madereva hao, ili kuepukana na ajali za kujitakia zitokanazo na uzembe wa madereva hao.
"Ipo haja kwa viongozi wa dini wawapo katika madhabahu wawakumbushe waumini wao juu ya kuzingatia sheria za usalama barabarani, kwani ajali ikitokea inawapoteza waumini wao, vivyo hivyo na wanasiasa nao wanapokuwa kwenye majukwaa wawakumbushea wapigakura wao ili watimize sheria za barabara," Alisema Mungi.
Akisoma lisara ya uongozi wa Polisi mkoa na kamati ya ulinzi na usalama, mwenyekiti wa chama cha waendesha pikipiki mkoa wa Iringa Joseph Mwambope amesema ili kutekeleza dhamira ya polisi jamii na ulinzi shirikishi kuna haja ya kuanzisha zoezi la kuwakamata madereva wote ambao hawana elimu ya mafunzo hayo.
Mwambope amesema pia serikali iwasaidie kupata wadhamini wa kuwakopesha fedha ili waweze kumiliki Pikipiki zao wenyewe, kwa madai kuwa asilimia kubwa ya madereva pikipiki hizo siyo zao, na hivyo huwawia vigumu kukidhi baadhi ya masharti zikiwemo kodi za manispaa zinazotakiwa kulipiwa mara tu dereva anapofanya kazi hiyo.
Aidha Mwambope amesema wamekuwa na ushirikiano mzuri baina ya uongozi wa chama cha bodaboda na jeshi la Polisi, lakini askari aitwaye Chande amekuwa ni kikwazo cha kazi yao na hata chama kushindwa kudhibiti matukio ya usafiri huo, kwa madai kuwa askari huyo amekuwa akipokea rushwa na kuruhusu Pikipiki zisizostahili kufanya kazi.
"Ndugu mgeni rasmi, kwa muda mrefu sasa kumekuwa na ushirikiano mzuri sana baina ya askari polisi na waendesha bodaboda na hata chama cha waendesha bodaboda, lakini kuna askari anayeitwa Chande- huyu amekuwa ni kikwazo kikubwa katika kumitiza makubaliano yetu na jeshi, kwani amekuwa ni msumbufu, huku akipokea rushwa kwa madereva, na pindi anaponyimwa basi dereva hupata taabu, tusaidie juu ya huyo Chande," Alisema.
Katibu wa chama hicho Ezekiel Lukosi amesema changamoto inayowakabiri ni pamoja na baadhi ya wenzao kutekwa na hata kuuawa na kunyang'anywa usafiri huo, na kupitia muungano huo watafanikiwa kudhibiti pia matukio hayo ya mauaji ya madereva wa bodaboda.
"Hili joho tulilovalishwa ni silaha toisha ya kutusaidia kwanza, kuhakikisha kipa pikipiki inayofanya kazi ya biashara ya usafiri inatambulika, kuanzia huko vijijini hadi hapa mjini wote tunaungana na kuwa kitu kimoja, tutafanikiwa kwa kiasi kikubwa, na pia hata kupunguza ajali, kwani tutawahimiza wenzetu ambao hawajapata elimu hii na hili tutafanikiwa kupitia chama chetu, kwani hatuatakubali pikipiki ifanye kazi bila dereva wake kupata elimu," Alisema Lukosi.
Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Salim Abri -Asas aliahidi kutoa Pikipiki za ulinzi shirikishi, zitakazosaidia kudhibiti vitendo vya uvunjifu wa usalama barabarani, kwa kuwawezesha viongozi wa madereva wa Bodaboda kufika katika matukio kwa wakati.
Asas ametoa nafasi 100 ya elimu kwa madereva ambao wanania ya kupata elimu ya kazi hiyo na wamekuwa wakikwamishwa na ada ya malipo ya kozi, na kuwa hatua hiyo ni kutoa fulsa kwa madereva wote wa Pikipiki kuwa na elimu ya kazi wanayoifanya kwa lengo la kutokomeza ajali.
Hata hivyo kamanda Mungi amemuagiza SP Zakaria Bernad ambaye ni askari mratibu wa Pikipiki mkoa wa Iringa kumsimamisha kazi PC Chande mara moja katika kitengo hicho ili kujenga ushirikiano baina ya chama cha waendesha Pikipiki na jeshi la Polisi kwa madai kuwa malalamiko dhidi ya madereva hao ni dhahiri kuwa askari huyo ni kikwazo cha usalama barabara.
"Kuanzia sasa huyo afande Chande simtaki
katika kazi hiyo, aende akafanye shughuli nyingine, kwani huku kwenye
Pikipiki ameonekana ni kikwazo, haiwezekani watu wote hawa zaidi ya 100
wakamlalamikia askari wetu mmoja tu huku wakiwapongeza wengine kwa kazi
nzuri, muondoe mara moja," Alisema Mungi.
Steven Nyatogo ambaye ni mkaguzi wa
vyombo vya moto na mwalimu wa vipindi vya usalama barabara alisema lengo
la mafunzo hayo endelevu kwa madereva wa pikipiki ni kuifanya kazi hiyo
itambulike katika jamii kutokana na mchango wake mkubwa katika sekta ya
uchumi.
Nyatogo amesema katika mkoa wa Iringa
madereva hao watapatiwa elimu, huku jeshi hilo likielekeza nguvu zake
pia katika maeneo ya pembezoni mwa mji, kwa kutoa mafunzo kwa madereva
na watumiaji wa usafiri wa Pikipiki Vijijini, lengo kuu likiwa ni
kutokomeza ajali za barabarani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni