VIONGOZI MKOANI IRINGA WAMPONGEZA MBUNGE WA VITIMAALUM MH.RITTA KABATI KWA KUPIGANIA MAENDELEO YA MKOA BUNGENI PIA WANANCHI WA MAENEO YA TUMAINI,SEMTEMA WATANUFAIKA NA KITUO KIPYA CHA POLISI
Viongozi mbalimbali mkoani iringa wamekutana kujadili suala la uboreshaji wa miundombinu (barabara) katika kikao cha bodi ya barabara kwa kushirikiana na mamlaka ya barabara TANROADS mkoa wa Iringa akiwemo mkuu wa mkoa Dr.Christine Ishengoma ambaye ndiye mwenyekiti wa kikao hicho,viongozi hao wamefikia maadhimio kadhaa ili kuongeza ufanisi na ukarabati wa barabara katika mkoa wa iringa ikiwa ni pamoja na utunzaji wa mazingira na usafi wamepitisha sheria ya kukaguliwa kwa magari yasiyokuwa na vyombo maarum kwaajili ya utupaji wa taka na gari yoyote itakayokamatwa ikiwa haina kifaa hicho itachukuliwa hatua ili kuwa fundisho kwa wengine,
Sambamba na hilo vingozi hao wamempongeza Mh.Ritta Kabati kwa kuwawakilisha vyema wanawake na wananchi wa mkoa wa Iringa hasa katika kupigania maendeleo ya mkoa,miongoni mwa mambo ambayo amekuwa akipigana nayo ni pamoja na Ukarabati wa miundombinu,elimu pamoja na Benki ya akina mama iliyoko Dar es Salam pekee ikiwa ni benki ya akina mama wote nchini hivyo amewataka viongozi wanaohusika na benki hiyo kuifikisha katika mkoa wa Iringa ili hata akina mama wa mkoa huu waweze kunufaika,
Wakati huohuo kutokana na kilio cha wanachi wa maeneo ya Tumaini,Semtema na maeneo jirani kudai kituo kidogo cha Polisi Mbunge huyo wa viti maalum mkoa wa Iringa Mh.Ritta Kabati amejitolea kujenga kituo cha Polisi katika maeneo hayo ili kuwasaidia wananchi wa maeneo hayo waliokuwa wakionelewa na watu wasio wema hivyo amesema kituo hicho kitaweza kusaidia kupunguza idadi ya uharifu katika maeneo hayo kwani kituo hicho ni moja kati ya vituo vingi vinavyohitajika mkoani ha Iringa.
Akimuonesha Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Bw.Athumani Mungi Mh.Kabati amemhakikishia kamanda kuwa ujenzi huo utakamilika mapema iwezekanavyo ili kuepusha adha kwa wananchi wa maeneo hayo,
Kwaupande waka kamanda wa Polisi mkoani hapa amempongeza Mbunge huyo kwa moyo wake wa kujitolea katika mambo ya jamii ambapo amesema Jeshi la Polisi linapenda kushirikiana na wadau wanaounga mikono jitihada za jeshi hilo katika kuboresha amani nchini huku akitoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano huo kwa umoja ni nguvu utengano ni Udhaifi.
Picha zote hapo chini zinaonesha ziara ya Mh.Mbunge na kamanda wa polisi mkoa wa Iringa katika kituo kidogo kinachojengwa.........................
|
Mh.Ritta Kabati Mbunge wa Vitimaalum akiwa katika eneo kinapojengwa kituo kipya Cha Polisi akiwa mdhamini wa kituo hicho. |
|
Mh.Ritta Kabati akiwa na kamanda wa polisi Mkoani Iringa Bw.Athumani Mungi eneo la kituo. |
|
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa kituo hicho cha Polisi eneo la Semtema |
|
Mwanamke fundi akijenga kituo kidogo cha Polisi |
|
Ukuta wa kituo cha Polisi ukijengwa na Mwanamke hiyo sawa |
|
Kamanda Athumani Mungi akielekezwa ramani ya jengo la kituo kidogo cha Polisi |
|
Dereva wa Mh.Mbunge kushoto akiwa eneo kinapojengwa kituo hicho cha Polisi |
|
Upande wa mbele wa kituo hicho |
|
Jengo |
|
Waandishi wa habari wakizungumza na Kamanda Mungi kuhusiana na ujenzi wa kituo hicho |
|
Kamanda Mungi akizungumza na wandishi wa habari huku akisifia ujenzi huo |
|
Gari ya kamanda wa polisi ikiwa mbele ya Jengo la polisi |
|
Mwanafunzi wa Chuo kikuu Tumaini Godfrey Mushi akizunguzia umuhim wa kituo hicho |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni