MBUNGE RITTA KABATI AFANIKISHA UNUNUZI WA VYOMBO VYA MUZIKI IHIMBO.
Jamii imeshauriwa kuwasaidia na kuwapenda watu wasio
jiweza na wanaoishi katika mazingira magumu.
Rai hiyo imetolewa na Mbunge vitimaalum mkoani
Iringa Mh.Ritta Kabari wakati akizungumza na waumini wa Kanisa la Kiinjiri la
Kilutheli Tanzania Usharika wa Ihimbo wilayani Kilolo mkoani Iringa ambapo
alikuwa mgeni rasmi katika halambee ya ununuzi wa vyombo vya muziki vya
usharika huomwishoni mwa wiki.
Akiwasilisha risala ya harambee hiyo kwaniaba
waumini na wanakwaya wa kanisa hilo mwalimu
Benard Simbeye ambeye pia ni mzee wa kanisa hilo amesema kanisa hilo
linakabiliwa na ukosefu wa vyombo vya muziki kwa muda mrefu kutokana na uhaba
wa fedha hivyo wamemuomba mbunge huyo kukwasaidia upatikanaji wa vyombo hivyo
ambavyo kwa ujumla vinaghalimu kiasi cha sh mil 4.5.
Akijibu risala hiyo Mh.Kabati amesema kwa kuwa
jukumu la kiongozi ni kuhakikisha jamii anayoiongoza inapata mahitaji ya msingi
ambapo katika harambee hiyo amewezesha kupatikana kwa fedha hiyo.
Aidha mh. Kabati amewataka wazazi kuwasomesha watoto
wao hususani wakike ili kusaidia jitihada za serikali za kuhakikisha kila
mtanzania anapata elimu.
Amewataka wazazi kuachana na Imani Potofu za kuwa mototo wa kike ni mtu wa kuolewa tabia ambazo baadhi ya wazazi wamekuwa wakilifanya jambo ambalo linawanyima watoto wa kike haki yao ya msingi ya kupata elimu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni