CHAMA CHA MAPINDUZI CCM BABA LAO

CHAMA CHA MAPINDUZI CCM BABA LAO
HII NDIYO CCM

Alhamisi, 22 Agosti 2013

Rais Kikwete ahudhuria kuapishwa kwa Rais Mugabe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kesho, Jumatano, Agosti 22, 2013 mjini Harare.

Rais Kikwete na ujumbe wake ameondoka nchini jioni ya leo, Jumatano, Agosti 21, 2013, kwenda Harare kuhudhuria sherehe hizo zinazofuatia ushindi wa Rais Mugabe na chama chake cha ZANU-PF katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini humo Julai 31, mwaka huu, 2013. Katika uchaguzi huo, Rais Mugabe alipata asilimia 61 ya kura zote.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
21 Agosti, 2013


WAHUDUMU WA ZAHANATI WATUHUMIWA KUFANYA NGONO NA WAGONJWA

Watumishi wawili katika zahanati ya Mwanhala wilayani Nzega, wamekumbwa na kashfa ya kufanya mapenzi na wagonjwa hospitalini.

Kutokana na kashfa hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Bitun Msangi, ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, kuchukua hatua kali za kinidhamu kwa watumishi hao.

Agizo la mkuu huyo limetolewa hivi karibuni, baada ya Diwani wa kata ya Utwigu, Sawaka Shita kuwalalamikia watumishi hao mbele ya Baraza la Madiwani, kwa kukithiri kufanya mapenzi na wagonjwa nyakati za kazi, licha ya kuonywa kwa mara kadhaa.

Diwani huyo aliliambia baraza hilo kuwa vitendo hivyo vinahatarisha maisha ya watumishi hao  na ya 
wananchi, hususani waliotembea nao na kutishia kuvunja ndoa za wananchi.

Alidai kuwa taarifa hizo za malalamiko, zilishafika katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, tayari kwa utekelezaji, lakini  wananchi wa kata hiyo walitaka kuifunga zahanati hiyo, baada ya kukithiri vitendo hivyo vya kufanya mapenzi katika wodi zilizopo.

Aliomba baraza liwahamishe na kuwachukulia hatua kali za kinidhamu  watumishi hao, ambapo majina yao yamehifadhiwa kwa usalama wao, huku jitihada za kuwachukulia hatua  zikifanyika.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Patric Mbozu alisema  suala hilo ni la hatari na linapaswa kufuatiliwa kwa umakini ili lipatiwe ufumbuzi na  wananchi waendelee kupatiwa huduma za tiba.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Abraham Mdeme alikiri kupokea malalamiko hayo na kuahidi kuwa suala hilo, litafuatiliwa mapema ikiwemo kuwahamisha kwa kufuata taratibu zilizopo.

Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Msangi alisema watumishi hao, wamevunja maadili ya afya, hususani kufanya ngono katika wodi za zahanati kwa nyakati za kazi.
 
ombeni_b1b00.jpg
Rais Jakaya Kikwete amefanya uteuzi wa makatibu wakuu kumi na mmoja na naibu makatibu wakuu 14 wapya katika wizara mbalimbali.Miongoni mwa walioteuliwa ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Profesa Sifuni Mchome ambaye sasa anakuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na aliyekuwa Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deodatus Mtasiwa ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu, Tamisemi.
P.T
Mtasiwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni walisimamishwa kazi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda Februari, mwaka jana kupisha uchunguzi dhidi yao, kutokana na kukithiri kwa migomo ya madaktari nchini, pamoja na utendaji wao kulalamikiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue alisema: "Mtasiwa ameteuliwa kwa kuwa uchunguzi dhidi yake haujaonyesha kuwa ana kosa lolote, lakini wenzake (Nyoni) na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo bado wanachunguzwa.
Katika uteuzi huo, aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo amehamishiwa Ikulu kusimamia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), kuwa Naibu Mtendaji Mkuu mwenye jukumu la kuanzisha na kuongoza Idara ya Mageuzi ya Kilimo.
Makatibu wakuu walioachwa kwa maelezo kuwa watapangiwa kazi nyingine ni Sethi Kamuhanda (aliyekuwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo), Kijakazi Mtengwa (Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto) na Omary Chambo (Uchukuzi), huku aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa akistaafu wa hiari.
Balozi Sefue alisema Rais Kikwete ameanzisha kitengo kipya katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), kitakachokuwa kikishughulikia afya ambacho kitasimamiwa na Dk Mtasiwa.
Aidha, aliwataja makatibu wakuu waliohamishwa wizara kuwa ni Florens Turuka kutoka Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwenda Ofisi ya Waziri Mkuu na Joyce Mapunjo kutoka Viwanda na Biashara kwenda Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Makatibu wakuu wapya
Alisema Jumanne Sagini ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo.
Dk Servacius Likwelile ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo. Dk Patrick Makungu ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Tekinolojia pia ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo.
Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Alfayo Kidata ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Dk Shaaban Mwinjaka aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi. Uledi Mussa ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko.
Charles Pallangyo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu sasa anakuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya. Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Anna Maembe ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo.
Sihaba Nkinga ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana na Utamaduni ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo na Sophia Kaduma ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika pia ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo.
Naibu makatibu wakuu wapya
Naibu makatibu wakuu wapya wizara zao katika mabano ni Angelina Madete (Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira), Regina Kikuli (Ofisi ya Waziri Mkuu), Zuberi Samataba (Ofisi ya Waziri Mkuu-Tamisemi anayeshughulika na Elimu), Edwin Kiliba (Ofisi ya Waziri Mkuu-Tamisemi), Dk Yamungu Kayandabila (Kilimo, Chakula na Ushirika), Profesa Adolf Mkenda (Fedha-Sera), Dorothy Mwanyika (Fedha-Fedha za Nje na Madeni), Rose Shelukindo (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa), Dk Selassie Mayunga (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi), Monica Mwamunyange (Uchukuzi).
Consolata Mgimba (Elimu na Mafunzo ya Ufundi), Profesa Elisante ole Laizer (Habari, Utamaduni na Michezo) na Armantius Msole (Ushirikiano wa Afrika Mashariki).
Waliohamishwa
Naibu makatibu wakuu waliohamishwa ni John Mngodo (Uchukuzi kwenda Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Selestine Gesimba (Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwenda Wizara ya Maliasili na Utalii).
Injinia Ngosi Mwihava (Ofisi ya Makamu wa Rais kwenda Wizara ya Nishati na Madini), Maria Bilia (Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwenda Viwanda na Biashara na Nuru Milao (Maliasili na Utalii kwenda Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto).
Aidha, Dk Donaldo Mbando amethibitishwa kuwa Mganga Mkuu wa Serikali baada ya kukaimu nafasi hiyo tangu kusimamishwa kwa Dk Mtasiwa.


WANANCHI KILOMBERO WANUFAIKA NA MRADI WA MAJI YA VISIMA 

Akina mama wa Kilombero wakiandaa mlo kwa ajili ya timu za Help for Underserved Communities (HUC) na Lifetime Wells for Ghana Inc., wakati wa ufungaji pampu katika moja ya visima Wilaya ya Kilombero, Morogoro, uliofanyika hivi karibuni. Zaidi kuhusu mradi huu bofya; www.facebook.com/pages/Help-for-Underserved-Communities-HUC-USA. (Picha zote na Nathan Mpangala wa HUC)
P.T

pic_2_27474.jpg
Mtoto toka Kilombero, akifuatilia ufungaji pampu katika moja ya visima 59 uliofanywa na timu za Help for Underserved Communities (HUC) na Lifetime Wells for Ghana Inc., Wilaya ya Kilombero, Morogoro, hivi karibuni.
Haya twende! Timu ya Help for Underserved Communities (HUC) ikishirikiana na Lifetime Wells for Ghana Inc., wakichimba moja ya visima 59 Wilaya ya Kilombero, Morogoro, huku wakiangaliwa kwa shauku na watoto hivi karibuni. HUC ni asasi isiyokuwa ya kiserikali yenye makao yake Marekani, inayochimba visima kwa kushirikiana na jamii kusaidia upatikanaji wa maji ya kunywa safi na salama mashuleni, vijijini na jamii kwa ujumla. Zaidi, bofya; www.facebook.com/pages/Help-for-Underserved-Communities-HUC-USA.

Mwanasiasa wa Sweden ajeruhiwa Somalia;

anna_magarethe_livh_304x171_bbc_nocredit_439a6.jpg
Watu waliokua na silaha wamewaua watu wawili na kumjeruhi mwanasiasa wa Sweden Ann-Margarethe Livh baada ya kushambulia gari lake mjini Mogadishu, Somalia.
Maafisa wanasema watatu hao walishambuliwa wakati wakirejea katika hoteli ya mwanasiasa huyo baada ya kutoa hotuba kuhusu demokrasia katika chuo kikuu mjini humo.
P.T

Hakuna kundi lililodai kutekeleza shambulio hilo wala sababu za kumlenga Bi Livh. Somalia inakabiliwa na maasi ya wanamgambo wa kiisilamu wa Al Shabaab ambapo pia inakumbwa na visa vya jinai.
Wiki jana shirika la misaada la Medecins Sans Frontier{MSF} lilitangaza kufunga huduma zake zote nchini Somalia kutokana na mashambulio dhidi ya wafanyikazi wake.
Somalia imekua bila serikali thabiti tangu kuondolewa madarakani kwa utawala wa Siad Barre mwaka wa 1991.
Duru za usalama zimesema Bi Livh amepokea matibabu katika hospitali ya wanajeshi wa Muungano wa Afrika mjini Mogadishu. Msemaji wa chama cha Ann-Mararethe Livh amesema mwanasiasa huyo alipata majeraha ya risasi.
Kwa sasa kuna mipango ya kumsafirisha hadi mjini Nairobi, Kenya kwa matibabu zaidi.Familia yake imesema mwanasiasa huyo alikua shwari licha ya majeraha.
Takriban wanajeshi 18,000 wa Muungano wa Afrika wanashika doria nchini Somalia ili kusaidia serikali mpya ya Somalia. Utawala wa sasa ndio wa kwanza kutambuliwa na Umoja wa Mataifa, Marekani na Shirika la Fedha duniani kwa zaidi ya miongo miwili.
Wapiganaji wa Al Shabaab wameondolewa mjini Mogadishu lakini wanathibiti maeneo kadhaa ya Somalia. Kuna makundi mengine ya kikoo ambayo yanathibiti maeneo mengi ya Somalia.

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni