Mh.mbunge Ritta Kabati akikabidhi fedha tasilimu kwa wanavikundi ikiwa ni sehemu ya utekeklezaji wa ahadi zake kwa vikundi vya wajasiliamali
Wanavikundi |
Haya yamesemwa mapema hii leo na naibu mstahiki meya wa manispaa ya Iringa Bwana Gervas Ndaki alipokuwa akiongea na vikindi vya akinamama wajasiriamali wa VICOBA vilinyokuwa vikipokea msaada waliyoahidiwa na mbunge wa viti maalum mh Ritha Kabati katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa halimashauri ya manispaa ya Iringa .
Ndaki amesema kuwa amekuwa akisikitishwa na kauli za viongozi hao waliochaguliwa kwa kura za wananchi wakiwakashfu kwa kusema kuwa wao siyo ATM za benki za kugawa pesa kwa kila mtu mwenye matatizo jambo linaloonyesha zarauu kubwa na kubweteka kwa madara waliyokwishakuyapata
Amesema kuwa viongozi hao wanapaswa kuwasikiliza wanchi hao kwa ukarimu na upole na kujiribu kutatua matatizo yao na kuwataka kuiga mfano wa mh Ritha ambaye si mbunge wakuchaguliwa na wananchi bali amekuwa mstari wa mbele kusaidi watu mabalimbali vikiwemo vikundi vya ujasiriamali,yatima ha hata kujenga kituo cha polisi kitakachosaidia jamii nzima ya wana wa Iringa
Kwa upande wake mbunge Ritha amesema yeye siyo kwamba ni Tajiri kwa kutoa msaada mbalimbali bali amekuwa akijinyima posho zake za ubunge ili kuja kuisaidia jamii ya wanairinga kwa kujaribu kutatua baadhi ya kero ambazo zipo ndani ya uwezo wake ambapo katika kutekeleza ahadi zake kwa wajasiliamali hao zaidi ya shilingi milioni 5 zimetumika.
Mh.Ritha amesema kuwa kiongozi yoyotote aliyemwadilifu si mtu wa kukimbia changamoto au kulalamika bali anapaswa kuwa mastari wa mbele kuwa wa kwanza kutatua changamoto na ndipo wengine wafuate na siyo kulalamika na kupiga kelele bungeni bila ya kuchukua hatua za uthubutu
Hata hivyo wajasiriamali hao wamemshukuru mbunge huyo kwa kuwakumbuka watu wenye mahitaji mbalimbali na kuwataka viongozi wengine waige mfano wa mbunge huyo na siyo kuwageuza shuka la kisiasa pindi ifikapo kipindi cha chaguzi mbalimbali hapa nchini .
MH.RITTA KABATI MBUNGE WA VITI MAALUM MKOANI IRINGA AAHIDI KUENDELEZA MICHEZO MBALIMBALI KATIKA MKOA WA IRINGA.
Mh.Mbunge Ritta Kabati akiwa na baadhi ya viongozi wa michezo kata ya Ruaha Iringa |
Mh.Mbunge akiwa na Timu shiriki |
Mh.Mbunge akiwa na kijana aliyefanikiwa kuwa mchezaji bora katika mashindano |
Mh.Mbunge akikabidhi zawadi kwa washindi |
Aidha alitoa wito kwa wadau wengine wa michezo kujitokeza kusaidia ukuzaji wa michezo ili kuufanya mkoa wa Iringa ufahamike kisoka sambamba na hilo amepongeza juhudi za uongozi wa wa klabu ya Lipuli Iringa kwa jitihada zao za makusudi wanazozifanya ili kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri kisoka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni