WAJUMBE WA MKUTANO MKUU MAALUM WA UTPC WATAKA MASLAHI YA WAANDISHI KUPIGANIWA
Wajumbe wa bodi ya UTPC wakifuatilia hoja za wajumbe wa Rasmu ya katiba ya UTPC leo mjini Dodoma
Wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa UTPC
wakiwa katika mchakato wa utoaji wa maoni ya rasmu ya katiba mpya
ya UTPC unaoendelea mjini Dodoma
Mwenhyekiti wa IPC Bw Frank Leonard akiwa katika ukumbi wa mkutano huo
Mwenyekiti wa Lindi Abdulaziz Video akiwajibika
katibu wa Tanga Press Club Bi Lulu George akiwa katika mkutano huo
WAKATI
kilio kikubwa cha wanahabari nchini kikiwa
ni maslahi duni wanayolipwa na vyombo ,wajumbe wa
mkutano mkuu maalum wa umoja
wa vilabu vya
waandishi wa habari Tanzania (UTPC)
wameshauri katika katiba
mpya ya UTPC kutoa nguvu zaidi ya
UTPC kusimamia maslahi ya wanahabari nchini.
Hivyo wameshauri katiba mpya ya UTPC kuingizwa kifungu ambacho kitasimamia masilahi stahiki kwa wanahabari hapa nchini kutoka na chombo kilichopewa kuifanya kazi hiyo TUJ kutangazwa kufutwa rasmi kutokana na kupoteza sifa.
Aidha wajumbe hao walisema kuwa kuwepo kwa mtetezi wa kweli wa maslahi stahiki kwa mwanahabari itakuwa ni moja ya njia ya kuboresha taaluma ya habari hapa nchini na kumfanya mwanahabari kuheshimu na kuthamkini kazi yake .
Kwa upande wake Rais wa UTPC Keneth Simbaya alisema kuwa UTPC imeanza mchakato wa kuifufua TUJ ili kusaidia kusimamia maslahi ya wanahabari na kuwa mchakato wake unakwenda vema.
“ Tumeanza jitihada za kutetea maslahi ya waandishi wa habari nchini na tupo katika hatua nzuri ya kufikia malengo tuliyojiwekea”
Alisema shabaha ya UTPC ni kuona wanachama wake na wanahabari nchini wanafanya kazi hiyo kwa kujituma zaidi na kupata maslahi yanayotakiwa kwa kazi anayoifanya.
Katika hatua nyingine Bw Simbaya aliwataka viongozi hao wa vilabu kufanya kazi kwa kujituma ili kuboresha vilabu vyao na kuonya wale wanaoingia katika nafasi za uongozi kwa ajili ya kutafuta posho
Kwani alisema iwapo wapo viongozi wameingia katika uongozi kwa ajili ya posho ni vema wakajitathimini upya kabla ya kuendelea kuwa viongozi wa posho badala ya kuwa viongozi wa vilabu.
Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC, Abubakar Karsan akizungumzia kuhusu uwiano wa uongozi unaozingatia jenda na kuwa iwapo klabu kitakuwa na viongozi wasio zingatia jenda basi klabu hiyo itakuwa imepoteza sifa kwani lengo la UTPC ni kuwawezesha wanawake pia kuingia katika nafasi za uongozi .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni