*Awataka
kutoa michango ya maendeleo kwa jamii inayowazunguka
KATIBU Mkuu
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amewataka wawekezaji nchi
kujenga tabia ya kutoa michango ya maendeleo kwenye maeneo ambayo wamewekeza na
si kutoa michango ili kumfurahisha Rais
au Waziri Mkuu.
Kinana
alitoa kauli hiyo jana katika Kijiji cha Mwendakulima katika Wilaya ya Kahama
mkoani Shinyanga ikiwa ni siku yake ya kwanza ya ziara yake ambayo itakuwa kwa
Mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara ambapo akiwa eneo hilo alizungumzia umuhimu
wa wawezaji kujitahidi kufanya maendeleo kwa wananchi ambao wamewekeza kwenye
maeneo yao.
“Wawekezaji
wapo tayari kutoa hadi sh.milioni 200 wakiwa Dar es Salaam, Mwanza au Arusha,
lakini ushauri wangu kwao, ni vema wakachangia kwenye maeneo ambayo wamewekeza
kwani hiyo itasaidia kuondoa malalamiko lakini pia itakuwa ni jambo jema
wananchi kunufaika kutokana na uwekezaji huo.
Alisisitiza
kuwa anatambua umuhimu wa wawekezaji kuchangia maendeleo lakini inapendeza
zaidi inapofika mahali wananchi wakawa
na maendeleo kutokana na wawekezaji.
Kinana
alifafanua hayo zaidi wakati akizindua kituo cha afya kwenye kijiji hicho
ambacho kimejengwa na kampuni ya madini ya Buzwagyi ambapo alisema kampuni hiyo
imeanza na eneo la afya lakini mwaka mwingine wanaweza kujenga miundombinu ya
barabara na mwaka unaofuata kufanya jambo lingine la maendeleo.
Wakati huo
huo Katibu Mkuu huyo , alisema kuwa Watanzania wanatakiwa kushiriki kikamilifu
kwenye mchakato wa Katiba mpya na kwamba msimamo wa chama chake ni Serikali
mbili lakini wapo tayari kwa uamuzi ambao utafanywa na wananchi kwa kuamua aina
ya katiba ambayo wanahitaji.
Pia alisema
wananchi wafahamu kuwa licha ya umuhimu wa kuwa na Katiba mpya lakini hiyo
haitakuwa mbadala wa kuwa na mabadiliko ya maisha baada ya kupatikana kwake
ambapo alitoa mifano ya nchi kadhaa Afrika na Asia ambazo zilipata katiba mpya
lakini hali ya uchumi kwa watu wake imebaki kuwa ile ile.
Akifafanua
kuhusu msimamo wa CCM wa kutaka muundo wa Serikali mbili, Kinana alisema hakuna
sababu ya kuwa na Serikali ya tatu kwani kuwanayo ni kuongeza mizigo kwa
Mtanzania kwani ni gharama kuindesha kwake lakini pia haitakuwa na kazi.
Pia Kinana
akiwa Kahama alizindua Saccos ya Mkombozi katika eneo la Isaka ambapo alitumia
nafasi hiyo kuwahimiza wananchi kubuni miradi ya maendeleo lakini pia kwa
vijana kujiendeleza kielimu hasa kusoma masomo ya ufundi yakiwamo ya ujenzi,
ufundi mchundo na aina nyingine nyingine ya taaluma ya ufundi ambayo
itawawezesha kupaa kipato.
Katika
kuhakikisha hilo la masomo ya ufundi linafanikiwa,Kinana aliweza kutoa ahadi ya
kusomesha vijana 10 wa eneo la Kahama na kwamba kama gharama itakuwa nafuu
ataongeza idadi ya vijana ikiwa ni sehemu ya kufanikisha malengo ya vijana.
Wakati huo
huo akiwa katika Uwanja wa CDT Kinana aliwataka Watanzania kuwa makini na
wapinzani kwani nia yao si kuwaisaidia Watanzania bali n kutafuta maslahi yao
na ndio maana wapo tayari kufanya lolote kufanikisha kile wanachokitaka.
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria kukamilika
kwa awamu ya kwanza ya jengo la kituo cha afya cha kijiji cha
Mwendakulima ambalo limedhaminiwa na Mgodi wa Buzwagi.
Septemba
7, 2013 nilipokea barua pepe (email) yenye kichwa cha habari kisemacho
“ubinafsi/ufisadi wa MENGI na Chuki/Fitina kwenye Maendeleo”.
Aliyetuma
email hiyo alijitambulisha kama “CCM TANZANIA” na email ilisambazwa kwa
vyombo vya habari, waandishi na watu wengine wengi wakiwamo wanasiasa.
Kabla ya hapo nilifowadiwa nakala ya ujumbe (SMS) na watu ambao
walitumiwa na Profesa Sospeter Muhongo, Waziri wa Nishati na Madini na
Mbunge inayosema;
|
“Ambieni
Watanzania: Kampuni za Mengi zimeshikilia vitalu 59 vya madini vyenye
ukubwa wa mita za mraba 3,752.37 (sq km) Amevishikilia, ameshindwa
kuviendeleza.
Watanzania wanakosa mapato na ajira! Sasa anataka vitalu
vya gesi na mafuta. Je huu ndio uzawa?|
|
|
Na
|
“Mengi hana uzawa bali ubinafsi. Anataka kufanya udalali wa vitalu vya raslimali zetu. Waelezeni Watanzania ukweli huu.”
|
|
Vile vile Septemba 5, 2013 Profesa Muhongo akijibu swali la Mwandishi wa habari lililouliza;
|
“Mhe.
Waziri tunataka ufafanuzi kuhusu kauli yako ya hivi karibuni kwamba
waTanzania hawana uwezo wa kuwekeza katika uwekezaji wa gesi asilia.
Kwanza kauli hii ni kweli? Pili kauli kwamba Watanzania wanaweza
kuwekeza kwenye sekta ya machungwa tu huoni kwamba si kwamba unawavunja
moyo bali unadhalilisha wewekezaji wazalendo?”
|
|
Na Profesa Muhongo akajibu:
|
“Kila
mtu alitoa mawazo ya sera ya gesi wakiwemo TPSF. Mengi na wenzake
wanataka vitalu wafanye ulanguzi wa gesi na mafuta yetu. Tutatoa orodha
ya vitalu vya madini vilivyoko mikononi wa Mengi ambavyo anafanya
ulanguzi. Ukweli utaonyesha ubabaishaji na ulanguzi wa Mengi wa genge
lake.”
|
|
Nimeona
ni vyema nitumie haki yangu ya kujibu (right of reply), lakini kwa wale
wanaohusika kusambaza taarifa hizo kuchafua jina langu wajue kwamba
kujibu kwangu hakuondoi haki yangu ya kuchukua hatua za kisheria.
Kuingizwa kwa vitalu vya madini katika hoja ya gesi
Huo
ni upotoshwaji wenye lengo la kututoa kwenye hoja ya msingi ya
rasilimali yetu ya gesi. Sijawahi kufanya udalali kwenye vitalu vya
madini. Huu ni uongo wa hali ya juu.
Tamko la TPSF na majibu ya Profesa Muhongo
Siku
ya Agosti 28, 2013 Tanzania Private Sector Foundation (TPSF) ilifanya
kikao chake cha Bodi na baadaye kufanya mkutano na waandishi wa habari.
Mambo mengi yalizungumzwa katika kikao hicho ikiwa ni pamoja na
uwezeshaji wa Watanzania (Economic Empowerment).
Kuhusu
uwezeshaji Watanzania, mambo muhimu matatu yalijadiliwa na kutolewa
mapendekezo. Mambo hayo ni 1) Manunuzi ya Umma (Public Procurement); 2)
Ardhi na uvuvi; na 3) suala la gesi asilia.
Kwenye
mkutano na waandishi wa habari, mimi nikiwa Mwenyekiti wa TPSF,
niliwasilisha maoni ya TPSF kuhusiana na Manunuzi ya Umma, wakati Makamu
Mwenyekiti wangu, Salum Shamte, aliwasilisha maoni yetu kuhusiana na
sekta ya ardhi na uvuvi na mwishoni Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey
Simbeye, aliwasilisha maoni TPSF kuhusiana na gesi asilia.
Katika
maoni yake TPSF ilisisitiza umuhimu wa ushirikishwaji wa Watanzania
katika uchumi wa gesi na kushauri kusitishwa ugawaji wa vitalu vya gesi
hadi hapo sera ya gesi itakapokua tayari. Mwisho Bwana Simbeye alisema
kwamba TPSF itaomba kukutana na Profesa Muhongo kuwasilisha mawazo na
mapendekezo ya taasisi hiyo.
Siku
chache baada ya TPSF kutoa maoni yake mambo mawili yalitokea. Kwanza
Profesa Muhongo alijibu kupitia vyombo vya habari kwamba mpango wa
kugawa vitalu vya gesi na kuingia mikataba utaendelea.
Profesa Muhongo pia alisema wazi kwamba hana mpango wa kukutana TPSF, kwani kufanya hivyo ni kupoteza muda.
Matokeo
yake Profesa Muhongo hajajibu hoja kuhusiana na barua aliyoandikiwa na
TPSF. Binafsi nilishitushwa na msimamo wa Profesa Muhongo kwani Serikali
ya awamu ya nne imepiga hatua kubwa katika kudhihirisha kuwa ni
“serikali sikivu”. Ingemgharimu nini Profesa Muhongo kukaa na
kutusikiliza? Hakuna ambacho angepoteza zaidi ya dakika chache za muda
wake.
Jambo
la pili ambalo lilitokea ni mimi binafsi kushambuliwa kana kwamba maoni
yaliyotolewa kuhusiana na gesi ni maoni yangu binafsi na si ya TPSF.
Mifano ya mashambulizi dhidi yangu ni kama nilivyoonyesha hapo juu katika email na ujumbe mfupi wa simu (SMS).
Msimamo wa Profesa Muhongo katika gesi ni upi?
Msimamo
wa Profesa Muhongo mara baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na
Madini ulikuwa ni kutaka kupitishwa kwanza kwa sera ya gesi asilia kabla
ya kuendelea na ugawaji wa vitalu vya gesi.
Septemba 2012, Profesa Muhongo alisema;
“Some of the agreements are really shoddy and they need to be revoked” and “I can’t tolerate agreements which are not in the country’s interests but they benefit a few individuals”.
|
Tafsiri yake ni:
|
“Baadhi
ya mikataba ni ya ovyo, na inahitaji kuvunjwa” na “Sitovumilia mikataba
ambayo haina maslahi kwa nchi na inawanufaisha wachache”.
|
Baada
ya hapo, Profesa Muhongo aliamrisha Bodi mpya ya TPDC kusitisha ugawaji
wa vitalu vya gesi ambao ulipangwa kufanyika mwezi Septemba 2012 na
kupitia upya mikataba yote. Profesa Muhongo alinukuliwa akisema:
|
‘Earlier
this month, the state-run Tanzania Petroleum Development Corporation
(TPDC) delayed a licensing round for nine deep-sea oil and gas blocks
previously set for this month until a parliamentary vote on a new gas
policy in October. "Right now as a country, we are in the gas boom and
we don't have gas policy in place.”
|
|
|
[…]
|
|
|
Recent
gas strikes off east Africa's seaboard have led to predictions the
region could become the third largest exporter of natural gas on the
planet.
|
|
|
"Our
country is reviewing its policy. Is that something new?" he said. "We
want both the companies that are investing in the country and Tanzanians
to benefit from the oil and gas projects."
|
|
|
[…]
|
|
|
"This is completely new business to us. We are learning," Muhongo said.’
|
|
Tafsiri yake ni:
|
|
|
|
‘Mwanzoni
wa mwezi huu TPDC ilihairisha mchakato wa ugawaji wa vitalu tisa vya
gesi asilia vilivyoko baharini hadi hapo Bunge litakapopitisha sera mpya
ya gesi iliyowasilishwa bungeni mwezi Oktoba;
"Kwa sasa kama Taifa, tuko katika mazonge ya gesi na hatuna sera ya gesi.
"Nchi yetu inaandaa sera (ya gesi). Hicho ni kitu kipya?..."
"Tunataka kampuni zote, kampuni zinazowekeza nchini mwetu na Watanzania tunufaike na miradi ya gesi na mafuta."
"Hii ni biashara mpya kabisa kwetu. Tunajifunza."
|
|
http://www.reuters.com/article/2012/09/18/tanzania-exploration-idUSL5E8KIPEJ20120918
Zoezi wa la kugawa vitalu vya gesi asilia lilisitishwa lakini hadi sasa matokeo ya kupitia upya mikataba hayajatolewa hadharani.
Miezi
michache baadaye, Februari 26, 2013, Profesa Muhongo alisisitiza
msimamo wake wa kutaka Tanzania kuwa na sera ya gesi kabla ya kugawa
vitalu zaidi. Aliyasema hayo alipokua akihutubia mkutano uliofanyika
Chatham House, mjini London. Mkutano huo uliopewa jina “Tanzania: An
Emerging Energy Producer”. Ulikuwa na madhumuni ya:
|
“Tanzania
is drawing growing attention as a pivotal country in East Africa for
oil and natural gas exploration, having led the region in terms of new
discoveries of natural gas in 2012. With known gas reserves of
approximately 7.5 billion cubic feet, the potential to transform
Tanzania's international standing and domestic electricity production is
considerable. However, recent protests against the construction of a
pipeline to Dar es Salaam highlight the challenges that Tanzania faces
in ensuring that the benefits of its natural resources are widely felt.
|
Tafsiri yake ni:
|
“Tanzania
inaonyesha kuja juu katika Afrika Mashariki kwa uvumbuzi wa mafuta na
gesi asilia baada ya kuongoza kwa uvumbuzi wa gesi asilia mwaka 2012.
Ikiwa na wastani wa futi za ujazo bilioni 7.5, ni dhahiri itasaidia
Tanzania kupaa katika anga za Kimataifa na kusaidia uzalishaji wa umeme
kwa matumizi ya ndani. Hata hivyo, vurugu za hivi karibuni kupinga
ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaam inaashiria changamoto mpya
ambazo Tanzania sasa inakabiliana nazo kuhakikisha kwamba manufaa ya
gesi asilia yanawafikia watu wengi zaidi wa chini.”
|
Alichowasilisha Profesa Muhongo katika mkutano huo kwa ufupi kinapatikana katika tovuti hii;
http://www.chathamhouse.org/events/view/189235
Kama
inavyonekana kwenye kiambatanisho, moja ya nyaraka aliyowasilisha
Profesa Muhongo inaonyesha kwamba mchakato wa kuanza ugawaji wa vitalu
ungeanza baada ya kupitishwa kwa sera ya gesi.
Hadi sasa hatuna sera ya gesi asilia.
Lakini jambo la kushangaza, Profesa Muhongo amebadilika na anataka vitalu vigawiwe kabla ya kuwapo kwa sera gesi.
Sababu za kubadilika kwa Profesa Muhongo hazina mashiko
Profesa
Muhongo amenukuliwa na gazeti la Daily News la Agosti 31, 2013 akieleza
sababu zake za kutaka vitalu vigawanywe kabla ya kupitishwa kwa sera ya
gesi. Sababu kuu alizozisema ni tatu; (1) Ushindani wa soko na majirani
zetu akitolea mfano wa Msumbiji (2) Sheria ya mwaka 1960 iliyoanzisha
TPDC na Sheria ya Petroli ya mwaka 1980 kwamba zinatosha kusimamia
ugawaji wa vitalu akimaanisha sera na sheria mpya zitafuata baada ya
ugawaji wa vitalu; na (3) Watanzania hawana uwezo wa kuwekeza katika
sekta hii akimaanisha waachiwe wageni peke yao.
Maelezo
kwamba tunashindana na Msumbiji haya halalishi ugawaji vitalu kabla ya
sera. Utafiti wa gesi asilia ni jambo linachokua muda mrefu, ndio maana
TPDC wanaingia kwenye mikataba ya muda mrefu (isiyozidi miaka 11 kwenye
utafiti na miaka 25 kwenye uchimbaji). Kwa hiyo kusubiri miezi michache
ili Bunge letu liidhinishe sera, haiwezi kuathiri ushindani wa
kibiashara. Hata nchi Msumbiji anayoizungumzia hivi sasa inapitia upya
mpango wake wa uwekezaji katika gesi asilia na kuingiza sera na sheria
mpya zitakazo simamia rasilimali hiyo. Katika mahojiano yaliofanyika na
jarida la Africa Report mwezi Julai mwaka huu, Naibu Waziri wa Nishati
wa Msumbiji, Mh. Abdul Razak Noormahomed, alisema madhumuni ya
mabadiliko hayo ni kuwapa kipaumbele wananchi wa Msumbiji.
Mohojiano haya yanapatikana katika anuani ifuatayo:
http://www.theafricareport.com/Interview/extractive-industry-the-goal-is-to-give-an-edge-to-mozambicans-noormahomed.html).
Kama
nilivyoeleza hapo juu, mara baada ya Profesa Muhongo kuingia wizarani
alisema kinaga ubaga kwamba sheria iliyopo haikidhi mahitaji ya sekta ya
gesi asilia ndiyo maana akasimamisha ugawaji wa vitalu vya gesi na
kuamrisha mikataba ipitiwe upya na sera ipatikane. Leo tunashuhudia
Profesa Muhongo akila matapishi yake na kusema kwamba sheria zile zile
alizoziponda sasa zinafaa.
Kauli
ya Profesa Muhongo kwamba wafanyabiashara wa Tanzania wanaweza tu
kushiriki biashara ya juisi na soda na hawana uwezo wa kushiriki katika
biashara ya gesi yao ni dharau.
Kigezo
gani Profesa Muhongo anatumia kutoa kauli ya jumla yenye kutawaliwa na
hisia? Amefanya utafiti gani kupima uwezo wa kifedha wa wafanyabiashara
wa kitanzania? Kwa taarifa yake, wapo wafanyabiashara wengi ambao
wanaweza kupata fedha kwa ajili ya kuchimba visima vya gesi.
Ni
dhahiri kwamba Profesa Muhongo anathamini tu kampuni za kigeni,
anasahau kwamba kuna mifano ya kuwapo kampuni za kigeni ambazo zimekua
zikifanya udalali hapa nchini kwa miaka mingi kwenye rasilimali za nchi
yetu ikiwa ni pamoja na madini na gesi.
Uzalendo wangu:
Ningependa
kupuuza tuhuma kwamba mimi si mzalendo Wantanzania wanafahamu ukweli.
Vile vile ningependa kupuuza tuhuma kwamba mimi ni mbinafsi na sipendi
maendeleo ya Watanzania wenzangu kwa hili pia Watanzania wanafahamu
ukweli
Kuhusu
Kilimanjaro Hoteli na mgogoro na Yussuf Manji n.k, mtizamo wako
unategemea wewe upo katika kundi lipi kati ya kundi safi la waadilifu au
kundi chafu la wala rushwa. Watanzania wanafahamu msimamo wangu kwenye
hili.
Mimi
sipingi kuwepo kwa wawekezaje wageni katika sekta ya gesi lakini kuna
mambo mawili napigania.
Kwanza Watanzania wanufaike na rasilimali yao ya
gesi na pili iwepo sera ya gesi inayotoa kipaumbele kwa Watanzania
Mimi
napenda maendeleo ya nchi yangu; kwa hiyo hata siku moja siwezi kupinga
uwekezaji ama ubia na wawekezaji. Ninachosimamia ni manufaa kwa nchi
yangu.
Tuhuma kwamba nafanya kampeni dhidi ya wizara
Tuhuma
kwamba nimeandaa kongamano kwa ajili ya vijana wa Chadema si za kweli.
Huu ni uzushi usio na kichwa wala miguu. Vile vile madai kwamba naitumia
vibaya vyombo vya habari vya IPP Media si ya kweli hata kidogo
ikizingatiwa kwamba hata mahojiano ya Profesa Muhongo kwa simu akiwa
Austria, yalirushwa na kituo cha redio cha Radio Stereo kinachomilikiwa
na kampuni yangu ya ITV-Independent Television Limited.
Hitimisho
Julai mwaka huu, Rais wa Marekani Barack Obama, alihitimisha ziara yake ya Kiserikali nchini Tanzania, kwa kusema;
|
“Ultimately the goal here is for Africa to build Africa for Africans.”
|
|
|
Akimaanisha kwamba, Hatimaye Lengo ni Africa kujenga Africa kwaajili ya Waafrica
|
|
Profesa Muhongo asipingane na ushauri huu mzuri.
Nimalizie
kwa kuwahakikishia Watanzania kwamba mashambulizi binafsi dhidi yangu
yenye nia mbaya ya kunishushia heshima hayatakaa yafanikiwe.
Wenu,
Dk. Reginald A. Mengi