Mbunge huyo katika kutekereza majukum ya kuwatumikia wananchi wa mkoa wa iringa alipa fulsa hiyo siku chache baada ya kutoka katika vikao vya Bunge mjini Dodoma.
Katika ziara hiyo Mh.Ritta alipata nafasi ya kuzungumza na wafungwa wa geraza hilo na kuwatia moyo kwa changamoto wanazozipata katika gereza hilo ambapo alisema kuwa yeye kama mama mwenye uchungu na mtoto anaumia kuona jamii ya watu wengi wakiwa katika mazingira hayo kwani sikila mtu ayeko gerezani alifanya kosa hata kama alifanya kosa kuna watu wapo nje wanatenda uovu zaidi kuliko makosa yaliyofanywa na wale waliofungwa.
Hivyo kattika mazungumzo hayo alitoa fulsa kwa wafungwa na mahabusu kutoa maoni yao katika maoni hayo alipata ombi la baadhi ya wafungwa wenye maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi waalioomba kulipiwa faini ya shilingi laki moja na elfu ishilini ili waweze kutoka pamoja na kukutana na Raia wa kigeni kutoka nchini Ethiopia 12 waliowekwa mahabusu katuka gereza hilo ambao wanahitaji kiasi cha shilingi elfu hamsini kila mmoja ambapo jumla ni shilingi laki sita ili kupunguza msongamono wa wafungwa waliopo katika gereza hilo kwani hivi sasa gereza hilo lina jumla ya wafungwa na mahabusu zaidi ya 400 ikiwa gereza hilo linaweza kuchukua wafungwa 228 pekee,hii ikiwa ni kwa mujibu wa mkuu wa Geraza hilo.
Kwa kushirikiana na viongozi wa juu serikalini akiwamo waziri wa sheria na waziri wa mambo ya Ndani Dk.Emmanuel Nchimbi na kuahidi kuzitekeleza baadhi ya changamoto zinazo likabili gereza hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni