CHAMA CHA MAPINDUZI CCM BABA LAO
Alhamisi, 14 Julai 2016
MBUNGE RITTA KABATI AKUTANA NA BARAZA LA WANAWAKE MANISPAA YA IRINGA ASISITIZA ELIMU YA MATUMIZI YA FEDHA.
Ni viongozi wa Katika jumuia ya wanawake mkoani iringa ambao hii leo viongozi hawa walikutana katika kikao cha kazi ili kujadili mambo mbalimbali yanayokikabili chama cha mapinduzi pamoja na namna ya kuimarisha chama chini ya Jumuiya hiyo ya wanawake UWT.
Miongoni mwa mambo yaliyozungumzwa katika kikao hicho ni pamoja na uwajibikaji wa viongozi katika maeneo yao ambapo pamoja na changamoto zilizopo wenyeviti na makatibu wa kata na mitaa katika manispaa ya Iringa wametakiwa kuanza kuitisha mabaraza ya wanawake katika maeneo yao ili kupata muda wa kuzungumza na kutafuta muafaka wa baadhi ya changamoto zilizopo kabla ya kuwasilisha katika balaza la wilaya au la mkoa.
Mgeni rasmi katika baraza hilo la jumuia ya wanwake manispaa ya iringa Mh.Zainabu Mwamwindi ambaye pia katika nafasi yake ya kiuongozi katika jumuia hiyo ni mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa pia ni Mbunge wa Viti maalumu kupitia jumuiya ya wazazi Taifa akiwakilisha mikoa 26 Tanzania Bara akitumia nafasi hiyo kuwafunda viongozi wa jumuiya hiyo katika kutengeneza timu ya pamoja itakayosababisha jumuiya hiyo kukua ambapo amewataka viongozi hao kila mmoja kwa nafasi yake kujipima kutokana na nafasi yake na kile anachokifanya katika eneo lake
Alisema katika uchaguzi ujao pamoja na nafasi za kuteuliwa koja kati ya vigezo vitakavyotumika katika kupitisha wagombea ni pamoja na kile kilichofanywa katika nafasi inayopita kutokana na baadhi ya viongozi kutowajibika ipasavyo na kushindwa kutetea maslahi ya chama hivyo nilazima kila kiongozi asimame katika nafasi yake kwa uhakika.
"nawaomba sana viongozi wenzangu tujenge moyo wa kujituma lakini pia tusimamie nafasi zetu kwa manufaa ya watanzania kwaujumla naamini mwisho wa uchaguzi ni mwanzo wa uchaguzi mwingine hivyo tunayokazi ya kufanya mbele yetu kutokana na hali halisi mnayoiona sasa Jumuiya ya wanawake pia inatajwa kuwa ndiyo pekee iliyofanya vizuri katika uchaguzi mkuu wa october 2015 pamoja na kupoteza jibu hili lakini bado nafasi ipo turudi tukajipange na tukaanze kuunda mabaraza ya mikakati ya ushindi"alisema mwenyekiti
Kwa upande wake mbunge wa vitimaalum mkoani Iringa Ritta Kabati pamoja na kuwashukuru wanawake kwa kumuombea alejee tena katika nafasi hiyo lakini amlisema dhamira yake ya kuwatumikia wananchi ipo palepale za kwa sasa nguvu itakuwa kubwa kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo pamoja na kuwasemea wananchi bungeni.
Ambapo pamoja na yote Mh Ritta kabati alitumia nafasi hiyo kuwaeleza juu ya mkakati wa serikali wa kuleta milioni 50 kwa kila kijiji ambapo amesema tayari mpango huo umepitishwa hivyo wananchi wajiandae ili pindi mpango huo utakapoanza kupelekwa vijijini wanawake wawekipaombele kunufaika na fedha hizo huku akiwaaasa kujiunga katika vikundi vya ujasiliamali ili fedha hizo ziwakute katika vikundi.
"ndugu zangu katika kulitambua suala la milioni 50 kila kijiji tayari nimeaanza mchakato wa kutekeleza ahadi yangu ya kujenga kituo cha mafunzo ya ujasiliamali pamoja na matumizi ya fedha ambacho kitakamilika muda si mrefu ambapo kitatoa elimu kwa watu wote bila kujali itikadi zao,hivyo tutapita kila kata kutoa elimu ya nn kinaendelea nchini"alisema Kabati
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)