Mbunge wa Vitimaalum mkoani Iringa Ritta Kabati alipotembelea familia ya watu watano wote wakiwa walemavu na wanaishi mazingira magumu Wilayani kilolo ambapo aahidi kuwajengea Nyumba ya Kisasa. |
Zikiwa zimebaki siku kadhaa
kumalizika kwa kipindi cha Uongozi wa wabunge hapa nchini hususani wabunge wa
Viti maalumu ambao wanatarajia kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo wananchi
na viongozi mkoani Iringa wampongeza Mbunge wa Viti maalumu Ritta Kabati.
Wakizungumza na Morning star redio
kwa nyakati tofauti wananchi hao wamempongeza Mh.Kabati kwa mchango wake kwa
jamii ya mkoa wa Iringa na kuonyesha moyo wa upendo na kuthamini ubora wa
maisha ya wanairinga wote bila kujali itikadi ya dini,siasa wa rangi ambapo
amekuwa akipigania maendeleo ya watu wa rika zote.
Wananchi hao wamemtaja Mbunge Kabati
kuwa ndiye kiongozi wa kuigwa na viongozi wengine kwa kuwa amekuwa amefanikiwa
kusemea vema mkoa wa Iringa na kutoa kero za wananchi bungeni bila woga na
kuifanya serikali kutekeleza kwa kuzingatia mchango wake.
Wakizitaja baadhi ya kazi
alizozifanya Mh.Kabati kuwa na pamoja na
kulipigania suala la haki sawa baina ya mwanamke na mwanaume,suala la kuwapa
elimu watoto wa kike ukizingatia katika ofisi ya mbunge huyo imekuwa ikisaidi
watoto wasiojiweza waliohitimu kidato cha nne kwa kuwatafutia vyuo mbalimbali
jambo ambalo limewafanya zaidi ya watoto elfu 15 kuendelea na masomo.
Aidha wamesema amekuwa akipigania
suala la miundombinu pamoja na afya ambapo kupitia jitihada zake zimesaidia
kuboresha wodi za wazazi katika Hospital ya wilaya ya Iringa sambamba na hilo
amejenga kituo cha polisi kwa ghalama ya Sh mil 45 kilichopo Semtema manispaa
ya Iringa.
Kwa upande wa viongozi akiwemo Meya
wa Halmashauri ya Iringa Amani Mwamwindi,Katibu wa CCM mkoa Hasani mtenga na
mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoani Iringa Wamempongeza kwa jitihada za
kuwezesha eneo la kihesa kilolo kuwa eneo la uendelezaji kwa makazi badala ya
kuwa eneo la hifadhi.