Mh Mbunge wa Vitimaalum Mkoani Iringa Ritta Kabati Azungumza na Viongozi wa Umoja wa Wanawake (UWT)wa kata zote za Wilayani ya Mufindi.
Mh.Mbunge Ritta Kabati Azungumza na Viongozi wa CWT Mufindi |
Baadhi ya Viongozi wa Wanawake Mufindi wakimsikiliza Mh Kabati |
Mbunge wa Vitimaalum Mkoani Iringa Ritta Kabati Azungumza na Viongozi wa CWT Mufindi alisema moja kati ya mambo ya mengi ya kuzingatia ni pamoja na Viongozi wenyewe kushiriki Katika chaguzi hizo pamoja na kuombea nafasi mbalimbali za uongozi ili kuweka usawa baina ya Wanawake na wanaume waliopo madarakani.
Alisema pamoja na jitihada za wabunge Wanawake bungeni akiwemo yeye kupigania usawa kwa wote wao kama Viongozi wa Wanawake wanaowajibu wa kuhamasisha jamii hususani Wanawake kushiriki Katika uchaguzi huo ili kuwapata Viongozi wanao wataka hususani wanaotokana na Chama cha Mapinduzi Chama tawala na Chama makini watakaowasaidia kutatua kero zao mbalimbali zinazowakabili.
Aidha aliwataka Viongozi hao kujitambua na kutambua majukumu yao kwa wananchi kama kuwatambua vyema wananchi wao na maeneo wanakoishi pia kutambua siku na eneo la kupiga kura siku hiyo na pia amewapongeza Wanawake wote waliojitokeza kuombea nafasi za uongozi zilizokuwa zinagombewa.
Aidha Mh Kabati amefanya ziara wilayani ya kilolo ambapo alizungumza na Viongozi wa Wanawake na kusisitiza Wanawake kushiriki chaguzi zinazowakabili ili kuongeza utendaji wao Kwani anaamini Wanawake wanaweza kuongoza maeneo mengi bila woga.
Pia amefanya ziara Halmashauri Manispaa ya Iringa na kufanya semina ya kuwaongezea uwezo wa utendaji Viongozi wa Wanawake Iringa Mjini ili kuendelea kukijenga chama kwa maendeleo ya wananchi.
Akimkaribisha Mh Kabati Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT Mufindi Bi Machelina Mkini amempongeza Mh Kabati kwa kuacha majukumu mengine na kufanya ziara kwa Wanawake wilayani humo hivyo amewataka Wanawake Wengine kumuunga mkono kwa majukumu aliyonayo.