CHAMA CHA MAPINDUZI CCM BABA LAO

CHAMA CHA MAPINDUZI CCM BABA LAO
HII NDIYO CCM

Ijumaa, 26 Julai 2013

MH.MBUNGE WA VITIMAALUM MKOA WA IRINGA RITTA KABATI AKIWA MKOANI KAGERA KATIKA UZINDUZI WA UWANJA WA NDEGE NA MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA.
Mh.Mbunge wa vitimaalum Ritta Kabati akisalimiana na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania J.K Kikwete wakati akiwasili mkoani Kagera kwa ziara


Jumanne, 9 Julai 2013

HONGERA MH.MBUNGE WA VITIMAALUM RITTA KABATI KWA KUSIKIA KILIO CHA WANANCHI.

VIONGOZI MKOANI IRINGA WAMPONGEZA MBUNGE WA VITIMAALUM MH.RITTA KABATI KWA KUPIGANIA MAENDELEO YA MKOA BUNGENI PIA WANANCHI WA MAENEO YA TUMAINI,SEMTEMA WATANUFAIKA NA KITUO KIPYA CHA POLISI

Viongozi mbalimbali mkoani iringa wamekutana kujadili suala la uboreshaji wa miundombinu (barabara) katika kikao cha bodi ya barabara kwa kushirikiana na mamlaka ya barabara TANROADS mkoa wa Iringa akiwemo mkuu wa mkoa Dr.Christine Ishengoma ambaye ndiye mwenyekiti wa kikao hicho,viongozi hao wamefikia maadhimio kadhaa ili kuongeza ufanisi na ukarabati wa barabara katika mkoa wa iringa ikiwa ni pamoja na utunzaji wa mazingira na usafi wamepitisha sheria ya kukaguliwa kwa magari yasiyokuwa na vyombo maarum kwaajili ya utupaji wa taka na gari yoyote itakayokamatwa ikiwa haina kifaa hicho itachukuliwa hatua ili kuwa fundisho kwa wengine,
Sambamba na hilo vingozi hao wamempongeza Mh.Ritta Kabati kwa kuwawakilisha vyema wanawake na wananchi wa mkoa wa Iringa hasa katika kupigania maendeleo ya mkoa,miongoni mwa mambo ambayo amekuwa akipigana nayo ni pamoja na Ukarabati wa miundombinu,elimu pamoja na Benki ya akina mama iliyoko Dar es Salam pekee ikiwa ni benki ya akina mama wote nchini hivyo amewataka viongozi wanaohusika na benki hiyo kuifikisha katika mkoa wa Iringa ili hata akina mama wa mkoa huu waweze kunufaika,

Wakati huohuo kutokana na kilio cha wanachi wa maeneo ya Tumaini,Semtema na maeneo jirani kudai kituo kidogo cha Polisi Mbunge huyo wa viti maalum mkoa wa Iringa Mh.Ritta Kabati amejitolea kujenga kituo cha Polisi katika maeneo hayo ili kuwasaidia wananchi wa maeneo hayo waliokuwa wakionelewa na watu wasio wema hivyo amesema kituo hicho kitaweza kusaidia kupunguza idadi ya uharifu katika maeneo hayo kwani kituo hicho ni moja kati ya vituo vingi vinavyohitajika mkoani ha Iringa.

Akimuonesha Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Bw.Athumani Mungi Mh.Kabati amemhakikishia kamanda kuwa ujenzi huo utakamilika mapema iwezekanavyo ili kuepusha adha kwa wananchi wa maeneo hayo,
Kwaupande waka kamanda wa Polisi mkoani hapa amempongeza Mbunge huyo kwa moyo wake wa kujitolea katika mambo ya jamii ambapo amesema Jeshi la Polisi linapenda kushirikiana na wadau wanaounga mikono jitihada za jeshi hilo katika kuboresha amani nchini huku akitoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano huo kwa umoja ni nguvu utengano ni Udhaifi.

Picha zote hapo chini zinaonesha ziara ya Mh.Mbunge na kamanda wa polisi mkoa wa Iringa katika kituo kidogo kinachojengwa.........................
Mh.Ritta Kabati Mbunge wa Vitimaalum akiwa katika eneo kinapojengwa kituo kipya Cha Polisi akiwa mdhamini wa kituo hicho.
Mh.Ritta Kabati akiwa na kamanda wa polisi Mkoani Iringa Bw.Athumani Mungi eneo la kituo.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa kituo hicho cha Polisi eneo la Semtema
Mwanamke fundi akijenga kituo kidogo cha Polisi
Ukuta wa kituo cha Polisi ukijengwa na Mwanamke hiyo sawa
Kamanda Athumani Mungi akielekezwa ramani ya jengo la kituo kidogo cha Polisi

Dereva wa Mh.Mbunge kushoto akiwa eneo kinapojengwa kituo hicho cha Polisi
Upande wa mbele wa kituo hicho
Jengo
Waandishi wa habari wakizungumza na Kamanda Mungi kuhusiana na ujenzi wa kituo hicho
Kamanda Mungi akizungumza na wandishi wa habari huku akisifia ujenzi huo
Gari ya kamanda wa polisi ikiwa mbele ya Jengo la polisi
Mwanafunzi wa Chuo kikuu Tumaini Godfrey Mushi akizunguzia umuhim wa kituo hicho



Jumanne, 2 Julai 2013

RAIS OBAMA KUTUA NCHINI


 RAIS WA MAREKANI BARACK OBAMA KULAKIWA NA MAMIA YA WATANZANIA KWA ZIARA YA SIKU MBILI

Rais Obama na familia yake wakiwasili katika uwanja wa ndege wa JK Nyerere nchini Tanzania

 
RaisDkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete  wakiwaongoza wageni wao Rais Barrack Obama wa Marekani na mkewe Michelle kuangalia ngoma mbalimbali za utamaduni muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere kwa ziara ya siku mbili nchini.
Rais Barrack Obama akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ)
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na mgeni wake Mama Michelle  Obama muda mfupi baada ya kuwasili kwa Rais Obama nchini kwa ziara ya siku mbili nchin.
Akina mama nao hawako nyuma kumlaki Barack Obama

Jumatatu, 1 Julai 2013


OFISI YA MBUNGE WA VITIMAALUM MKOA WA IRINGA MH.RITTA KABATI YACHANGIA SHILINGI LAKI MBILI KATIKA UZINDUZI WA ALBAM INAYOTAMBULIKA KWA JINA LA DHURUMA YAKE WADI MBWELWA AKA MTIMBILIKO ILIYOFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA KIHESA SOKONI 30/6/2013

Mgeni rasmi Mh Dorah Nziku Diwani wa viti maalum kwaniaba ya Mbunge wa vitimaalum mkoa wa Iringa Mh.Ritha Kabati  katika uzinduzi wa Albam ya Wadi Mbwelwa a k a Mtimbiliko


Mgeni Rasmi akiingia jukwaani

Wacheza show wakicheza wakati wa Uzinduzi
Wadi Mbwelwa A K A Mtimbiliko

Wadi na familia katika uzinduzi
Bandi ya Wadi Mtimbiliko Mbwelwa

mwimbaji wa nyimbo za injili Iringa Shiza Sanga katika uzinduzi
Bendi ya Jesus My Life ikitumbuiza katika uzinduzi wa albam ya Wadi Mtimbiliko

My Life Bendi
Kwaya ya Uinjilisti Kihesa KKKT
Miongoni mwa kwaya zilizoshiriki katika uzinduzi
Mimbaji wa nyimbo za Injili Manase akiimba katika Uzinduzi
Manase aikitunzwa baada ya kuufurahisha Umma


Jamii haikuwa Nyuma katika kumsindikiza Wadi Mbwelwa katika uzinduzi wa albam yake