CHAMA CHA MAPINDUZI CCM BABA LAO

CHAMA CHA MAPINDUZI CCM BABA LAO
HII NDIYO CCM

Alhamisi, 14 Julai 2016

MBUNGE RITTA KABATI AKUTANA NA BARAZA LA WANAWAKE MANISPAA YA IRINGA ASISITIZA ELIMU YA MATUMIZI YA FEDHA.



Ni viongozi wa Katika jumuia ya wanawake mkoani iringa ambao hii leo viongozi hawa walikutana katika kikao cha kazi ili kujadili mambo mbalimbali yanayokikabili chama cha mapinduzi pamoja na namna ya kuimarisha chama chini ya Jumuiya hiyo ya wanawake UWT.

Miongoni mwa mambo yaliyozungumzwa katika kikao hicho ni pamoja na uwajibikaji wa viongozi katika maeneo yao ambapo pamoja na changamoto zilizopo wenyeviti na makatibu wa kata na mitaa katika manispaa ya Iringa wametakiwa kuanza kuitisha mabaraza ya wanawake katika maeneo yao ili kupata muda wa kuzungumza na kutafuta muafaka wa baadhi ya changamoto zilizopo kabla ya kuwasilisha katika balaza la wilaya au la mkoa.

Mgeni rasmi katika baraza hilo la jumuia ya wanwake manispaa ya iringa Mh.Zainabu Mwamwindi ambaye pia katika nafasi yake ya kiuongozi katika jumuia hiyo ni mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa pia ni Mbunge wa Viti maalumu kupitia jumuiya ya wazazi Taifa akiwakilisha mikoa 26 Tanzania Bara akitumia nafasi hiyo kuwafunda viongozi wa jumuiya hiyo katika kutengeneza timu ya pamoja itakayosababisha jumuiya hiyo kukua ambapo amewataka viongozi hao kila mmoja kwa nafasi yake kujipima kutokana na nafasi yake na kile anachokifanya katika eneo lake

Alisema katika uchaguzi ujao pamoja na nafasi za kuteuliwa koja kati ya vigezo vitakavyotumika katika kupitisha wagombea ni pamoja na kile kilichofanywa katika nafasi inayopita kutokana na baadhi ya viongozi kutowajibika ipasavyo na kushindwa kutetea maslahi ya chama  hivyo nilazima kila kiongozi asimame katika nafasi yake kwa uhakika.
"nawaomba sana viongozi wenzangu tujenge moyo wa kujituma lakini pia tusimamie nafasi zetu kwa manufaa ya watanzania kwaujumla naamini mwisho wa uchaguzi ni mwanzo wa uchaguzi mwingine hivyo tunayokazi ya kufanya mbele yetu kutokana na hali halisi mnayoiona sasa Jumuiya ya wanawake pia inatajwa kuwa ndiyo pekee iliyofanya vizuri katika uchaguzi mkuu wa october 2015 pamoja na kupoteza jibu hili lakini bado nafasi ipo turudi tukajipange na tukaanze kuunda mabaraza ya mikakati ya ushindi"alisema mwenyekiti

Kwa upande wake mbunge wa vitimaalum mkoani Iringa Ritta Kabati pamoja na kuwashukuru wanawake kwa kumuombea alejee tena katika nafasi hiyo lakini amlisema dhamira yake ya kuwatumikia wananchi ipo palepale za kwa sasa nguvu itakuwa kubwa kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo pamoja na kuwasemea wananchi bungeni.

Ambapo pamoja na yote Mh Ritta kabati alitumia nafasi hiyo kuwaeleza juu ya mkakati wa serikali wa kuleta milioni 50 kwa kila kijiji ambapo amesema tayari mpango huo umepitishwa hivyo wananchi wajiandae ili pindi mpango huo utakapoanza kupelekwa vijijini wanawake wawekipaombele kunufaika na fedha hizo huku akiwaaasa kujiunga katika vikundi vya ujasiliamali ili fedha hizo ziwakute katika vikundi.
"ndugu zangu katika kulitambua suala la milioni 50 kila kijiji tayari nimeaanza mchakato wa kutekeleza ahadi yangu ya kujenga kituo cha mafunzo ya ujasiliamali pamoja na matumizi ya fedha ambacho kitakamilika muda si mrefu ambapo kitatoa elimu kwa watu wote bila kujali itikadi zao,hivyo tutapita kila kata kutoa elimu ya nn kinaendelea nchini"alisema Kabati

Jumatano, 3 Juni 2015

Itazame familia hii iliyotembelewa na Mbunge wa Vitimaalum Ritta Kabati wote wakiwa walemavu.

WANANCHI NA VIONGOZI WAMPONGEZA MBUNGE WA VITIMAALUM KWA JUHUDI ZAKE KATIKA KUPIGANIA MAENDELEO IRINGA.
Mbunge wa Vitimaalum mkoani Iringa Ritta Kabati alipotembelea familia ya watu watano wote wakiwa walemavu na wanaishi mazingira magumu Wilayani kilolo ambapo aahidi kuwajengea Nyumba ya Kisasa.
 

Zikiwa zimebaki siku kadhaa kumalizika kwa kipindi cha Uongozi wa wabunge hapa nchini hususani wabunge wa Viti maalumu ambao wanatarajia kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo wananchi na viongozi mkoani Iringa wampongeza Mbunge wa Viti maalumu Ritta Kabati.
Wakizungumza na Morning star redio kwa nyakati tofauti wananchi hao wamempongeza Mh.Kabati kwa mchango wake kwa jamii ya mkoa wa Iringa na kuonyesha moyo wa upendo na kuthamini ubora wa maisha ya wanairinga wote bila kujali itikadi ya dini,siasa wa rangi ambapo amekuwa akipigania maendeleo ya watu wa rika zote.
Wananchi hao wamemtaja Mbunge Kabati kuwa ndiye kiongozi wa kuigwa na viongozi wengine kwa kuwa amekuwa amefanikiwa kusemea vema mkoa wa Iringa na kutoa kero za wananchi bungeni bila woga na kuifanya serikali kutekeleza kwa kuzingatia mchango wake.
Wakizitaja baadhi ya kazi alizozifanya Mh.Kabati  kuwa na pamoja na kulipigania suala la haki sawa baina ya mwanamke na mwanaume,suala la kuwapa elimu watoto wa kike ukizingatia katika ofisi ya mbunge huyo imekuwa ikisaidi watoto wasiojiweza waliohitimu kidato cha nne kwa kuwatafutia vyuo mbalimbali jambo ambalo limewafanya zaidi ya watoto elfu 15 kuendelea na masomo.
Aidha wamesema amekuwa akipigania suala la miundombinu pamoja na afya ambapo kupitia jitihada zake zimesaidia kuboresha wodi za wazazi katika Hospital ya wilaya ya Iringa sambamba na hilo amejenga kituo cha polisi kwa ghalama ya Sh mil 45 kilichopo Semtema manispaa ya Iringa.
Kwa upande wa viongozi akiwemo Meya wa Halmashauri ya Iringa Amani Mwamwindi,Katibu wa CCM mkoa Hasani mtenga na mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake mkoani Iringa Wamempongeza kwa jitihada za kuwezesha eneo la kihesa kilolo kuwa eneo la uendelezaji kwa makazi badala ya kuwa eneo la hifadhi.

Jumanne, 2 Juni 2015



 MBUNGE RITTA KABATI AFANIKISHA UNUNUZI WA VYOMBO VYA MUZIKI IHIMBO.
Jamii imeshauriwa kuwasaidia na kuwapenda watu wasio jiweza na wanaoishi katika mazingira magumu.

Rai hiyo imetolewa na Mbunge vitimaalum mkoani Iringa Mh.Ritta Kabari wakati akizungumza na waumini wa Kanisa la Kiinjiri la Kilutheli Tanzania Usharika wa Ihimbo wilayani Kilolo mkoani Iringa ambapo alikuwa mgeni rasmi katika halambee ya ununuzi wa vyombo vya muziki vya usharika huomwishoni mwa wiki.

Akiwasilisha risala ya harambee hiyo kwaniaba waumini na wanakwaya wa kanisa hilo mwalimu   Benard Simbeye ambeye pia ni mzee wa kanisa hilo amesema kanisa hilo linakabiliwa na ukosefu wa vyombo vya muziki kwa muda mrefu kutokana na uhaba wa fedha hivyo wamemuomba mbunge huyo kukwasaidia upatikanaji wa vyombo hivyo ambavyo kwa ujumla vinaghalimu kiasi cha sh mil 4.5.

Akijibu risala hiyo Mh.Kabati amesema kwa kuwa jukumu la kiongozi ni kuhakikisha jamii anayoiongoza inapata mahitaji ya msingi ambapo katika harambee hiyo amewezesha kupatikana kwa fedha hiyo.

Aidha mh. Kabati amewataka wazazi kuwasomesha watoto wao hususani wakike ili kusaidia jitihada za serikali za kuhakikisha kila mtanzania anapata elimu.
 
Amewataka wazazi kuachana na Imani Potofu za kuwa mototo wa kike ni mtu wa kuolewa tabia ambazo baadhi ya wazazi wamekuwa wakilifanya jambo ambalo linawanyima watoto wa kike haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Jumatatu, 24 Novemba 2014

Mh Mbunge wa Vitimaalum Mkoani Iringa Ritta Kabati Azungumza na Viongozi wa Umoja wa Wanawake (UWT)wa kata zote za Wilayani ya Mufindi.
Mh.Mbunge Ritta Kabati Azungumza na Viongozi wa CWT Mufindi 
Baadhi ya Viongozi wa Wanawake Mufindi wakimsikiliza Mh Kabati
Viongozi wa Umoja wa Wanawake kutoka kata zote za Wilayani ya Mufindi wameaswa kushiriki kikamilifu Katikaiti uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanya December 14,2014 kote nchini ili kuwapata Viongozi wa serikali za mitaa wakiwepo wenyeviti wa mitaa.

 Mbunge wa Vitimaalum Mkoani Iringa Ritta Kabati Azungumza na Viongozi wa CWT Mufindi alisema moja kati ya mambo ya mengi  ya kuzingatia ni pamoja na Viongozi wenyewe kushiriki Katika chaguzi hizo pamoja na kuombea nafasi mbalimbali za uongozi ili kuweka usawa baina ya Wanawake na wanaume waliopo madarakani.

Alisema pamoja na jitihada za wabunge Wanawake bungeni akiwemo yeye kupigania  usawa kwa wote wao kama Viongozi wa Wanawake wanaowajibu wa kuhamasisha jamii hususani Wanawake kushiriki Katika uchaguzi huo ili kuwapata Viongozi wanao wataka hususani wanaotokana na Chama cha Mapinduzi Chama tawala na Chama makini watakaowasaidia kutatua kero zao mbalimbali zinazowakabili.

Aidha aliwataka Viongozi hao kujitambua na kutambua majukumu yao kwa wananchi kama kuwatambua vyema wananchi wao na maeneo wanakoishi pia kutambua siku na eneo la kupiga kura siku hiyo na pia amewapongeza Wanawake wote waliojitokeza kuombea nafasi za uongozi zilizokuwa zinagombewa.

Aidha Mh Kabati amefanya ziara wilayani ya kilolo ambapo alizungumza na Viongozi wa Wanawake na kusisitiza Wanawake kushiriki chaguzi zinazowakabili ili kuongeza utendaji wao Kwani anaamini Wanawake wanaweza kuongoza maeneo mengi bila woga.

Pia amefanya ziara Halmashauri Manispaa ya Iringa na kufanya semina ya kuwaongezea uwezo wa  utendaji Viongozi wa Wanawake Iringa Mjini ili kuendelea kukijenga chama kwa maendeleo ya wananchi.

Akimkaribisha Mh Kabati Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT Mufindi Bi Machelina Mkini amempongeza Mh Kabati kwa kuacha majukumu mengine na kufanya ziara kwa Wanawake wilayani humo hivyo amewataka Wanawake Wengine kumuunga mkono kwa majukumu aliyonayo.

Jumanne, 20 Mei 2014

HONGERA MH MBUNGE KWA KUPIGANIA HAKI WA WANANCHI WA IRINGA WOTE WANAKUOMBEA MAFANIKIO KWA KILA UNALOLIFANYA 

WANASEMA UBARIKIWE SANA.

Ijumaa, 3 Januari 2014

SEMINA YA WAJASILIAMALI WAKUBWA NA WAOGO TAREHE 13 NA 14 MWEZI HUU SIASA NI KILIMO

TANZANIA CHAMBER OF COMMERCE
INDUSTRY AND AGRICULTERE

Taarifa kwa wafanyabiashara ya kukuza Mitaji ya Biashara  

TCCIA Mkoani Iringa unawataarifu watu wote kuwa tarehe 13 na 14 January 2014 kutafanyika mafunzo ya Mpango wa kukuza Mitaji kupitia Dirisha la soko la Hisa la Dar es salam kwa wajasiriamali wadogo,wakati na wakubwa nchini.

Mfanyabiashara yeyote mwenye biashara au Unawazo la Biashara litakaloonesha kukua hdi kufikia kampuni yenye tija na kukuza Ajira au unataka kupanua Biashara yake lakini Mtaji ni tatizo anakaribishwa kushiriki Mafunzo hayo.

Fika Ujisajili katika ofisi ya TCCIA  Mkoa wa Iringa iliyopo Majengo ya RETCO mkabala na kituo cha mafuta Cha TFA 

MWISHO WA KUJIAJILI NI TAREHE 07/01/2014.

Kwa ufafanuzi zaidi wasiliana nasi kwa Simu 
0784 462307,0756 060561,0715 462307 na 026 2700071

Ijumaa, 20 Desemba 2013

WAETHIOPIA 12 WAPONEA MIKONONI MWA MBUNGE VITIMAALUM MKOANI IRINGA RITTA KABATI

MBUNGE WA VITIMAALUM AWAONDOA WAETHIOPIA 12 KUTOKANA NA MLUNDIKANO WA WAFUNGWA KATIKA GEREZA LA MKOA WA IRINGA NA UHITAJI WA KUPUNGUZA BAADHI YA WAFUNGWA KWA FAINI

Baada ya kutembelea katika Gereza la mkoa wa Iringa Mbunge wa Vitimaalumu Mkoani hapa alikutana na changamoto ya mlundikano wa wafungwa wengine wakiwa ni wageni raia wa Ethiopian 12 ambao kwa mujibu wa Mkuu wa Gereza hilo walitakiwa kulipiwa kiasi cha shilingi elfu hamsini 50,000/=ili watolewe kwakuwa nimiongoni mwa wafungwa wasiojihusihsa na jambo lolote katika gereza hilo hivyo Mbunge wa vitimaalum Ritta kabati kulipia fedha hizo na siku ya tarehe 18.12.2013 kufanikiwa kutolewa na kurudishwa nchini kwao ikiwa walishutumiwa kwa uhamiaji haram hapa nchini.