CHAMA CHA MAPINDUZI CCM BABA LAO

CHAMA CHA MAPINDUZI CCM BABA LAO
HII NDIYO CCM

Jumanne, 2 Juni 2015



 MBUNGE RITTA KABATI AFANIKISHA UNUNUZI WA VYOMBO VYA MUZIKI IHIMBO.
Jamii imeshauriwa kuwasaidia na kuwapenda watu wasio jiweza na wanaoishi katika mazingira magumu.

Rai hiyo imetolewa na Mbunge vitimaalum mkoani Iringa Mh.Ritta Kabari wakati akizungumza na waumini wa Kanisa la Kiinjiri la Kilutheli Tanzania Usharika wa Ihimbo wilayani Kilolo mkoani Iringa ambapo alikuwa mgeni rasmi katika halambee ya ununuzi wa vyombo vya muziki vya usharika huomwishoni mwa wiki.

Akiwasilisha risala ya harambee hiyo kwaniaba waumini na wanakwaya wa kanisa hilo mwalimu   Benard Simbeye ambeye pia ni mzee wa kanisa hilo amesema kanisa hilo linakabiliwa na ukosefu wa vyombo vya muziki kwa muda mrefu kutokana na uhaba wa fedha hivyo wamemuomba mbunge huyo kukwasaidia upatikanaji wa vyombo hivyo ambavyo kwa ujumla vinaghalimu kiasi cha sh mil 4.5.

Akijibu risala hiyo Mh.Kabati amesema kwa kuwa jukumu la kiongozi ni kuhakikisha jamii anayoiongoza inapata mahitaji ya msingi ambapo katika harambee hiyo amewezesha kupatikana kwa fedha hiyo.

Aidha mh. Kabati amewataka wazazi kuwasomesha watoto wao hususani wakike ili kusaidia jitihada za serikali za kuhakikisha kila mtanzania anapata elimu.
 
Amewataka wazazi kuachana na Imani Potofu za kuwa mototo wa kike ni mtu wa kuolewa tabia ambazo baadhi ya wazazi wamekuwa wakilifanya jambo ambalo linawanyima watoto wa kike haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Jumatatu, 24 Novemba 2014

Mh Mbunge wa Vitimaalum Mkoani Iringa Ritta Kabati Azungumza na Viongozi wa Umoja wa Wanawake (UWT)wa kata zote za Wilayani ya Mufindi.
Mh.Mbunge Ritta Kabati Azungumza na Viongozi wa CWT Mufindi 
Baadhi ya Viongozi wa Wanawake Mufindi wakimsikiliza Mh Kabati
Viongozi wa Umoja wa Wanawake kutoka kata zote za Wilayani ya Mufindi wameaswa kushiriki kikamilifu Katikaiti uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanya December 14,2014 kote nchini ili kuwapata Viongozi wa serikali za mitaa wakiwepo wenyeviti wa mitaa.

 Mbunge wa Vitimaalum Mkoani Iringa Ritta Kabati Azungumza na Viongozi wa CWT Mufindi alisema moja kati ya mambo ya mengi  ya kuzingatia ni pamoja na Viongozi wenyewe kushiriki Katika chaguzi hizo pamoja na kuombea nafasi mbalimbali za uongozi ili kuweka usawa baina ya Wanawake na wanaume waliopo madarakani.

Alisema pamoja na jitihada za wabunge Wanawake bungeni akiwemo yeye kupigania  usawa kwa wote wao kama Viongozi wa Wanawake wanaowajibu wa kuhamasisha jamii hususani Wanawake kushiriki Katika uchaguzi huo ili kuwapata Viongozi wanao wataka hususani wanaotokana na Chama cha Mapinduzi Chama tawala na Chama makini watakaowasaidia kutatua kero zao mbalimbali zinazowakabili.

Aidha aliwataka Viongozi hao kujitambua na kutambua majukumu yao kwa wananchi kama kuwatambua vyema wananchi wao na maeneo wanakoishi pia kutambua siku na eneo la kupiga kura siku hiyo na pia amewapongeza Wanawake wote waliojitokeza kuombea nafasi za uongozi zilizokuwa zinagombewa.

Aidha Mh Kabati amefanya ziara wilayani ya kilolo ambapo alizungumza na Viongozi wa Wanawake na kusisitiza Wanawake kushiriki chaguzi zinazowakabili ili kuongeza utendaji wao Kwani anaamini Wanawake wanaweza kuongoza maeneo mengi bila woga.

Pia amefanya ziara Halmashauri Manispaa ya Iringa na kufanya semina ya kuwaongezea uwezo wa  utendaji Viongozi wa Wanawake Iringa Mjini ili kuendelea kukijenga chama kwa maendeleo ya wananchi.

Akimkaribisha Mh Kabati Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT Mufindi Bi Machelina Mkini amempongeza Mh Kabati kwa kuacha majukumu mengine na kufanya ziara kwa Wanawake wilayani humo hivyo amewataka Wanawake Wengine kumuunga mkono kwa majukumu aliyonayo.

Jumanne, 20 Mei 2014

HONGERA MH MBUNGE KWA KUPIGANIA HAKI WA WANANCHI WA IRINGA WOTE WANAKUOMBEA MAFANIKIO KWA KILA UNALOLIFANYA 

WANASEMA UBARIKIWE SANA.

Ijumaa, 3 Januari 2014

SEMINA YA WAJASILIAMALI WAKUBWA NA WAOGO TAREHE 13 NA 14 MWEZI HUU SIASA NI KILIMO

TANZANIA CHAMBER OF COMMERCE
INDUSTRY AND AGRICULTERE

Taarifa kwa wafanyabiashara ya kukuza Mitaji ya Biashara  

TCCIA Mkoani Iringa unawataarifu watu wote kuwa tarehe 13 na 14 January 2014 kutafanyika mafunzo ya Mpango wa kukuza Mitaji kupitia Dirisha la soko la Hisa la Dar es salam kwa wajasiriamali wadogo,wakati na wakubwa nchini.

Mfanyabiashara yeyote mwenye biashara au Unawazo la Biashara litakaloonesha kukua hdi kufikia kampuni yenye tija na kukuza Ajira au unataka kupanua Biashara yake lakini Mtaji ni tatizo anakaribishwa kushiriki Mafunzo hayo.

Fika Ujisajili katika ofisi ya TCCIA  Mkoa wa Iringa iliyopo Majengo ya RETCO mkabala na kituo cha mafuta Cha TFA 

MWISHO WA KUJIAJILI NI TAREHE 07/01/2014.

Kwa ufafanuzi zaidi wasiliana nasi kwa Simu 
0784 462307,0756 060561,0715 462307 na 026 2700071

Ijumaa, 20 Desemba 2013

WAETHIOPIA 12 WAPONEA MIKONONI MWA MBUNGE VITIMAALUM MKOANI IRINGA RITTA KABATI

MBUNGE WA VITIMAALUM AWAONDOA WAETHIOPIA 12 KUTOKANA NA MLUNDIKANO WA WAFUNGWA KATIKA GEREZA LA MKOA WA IRINGA NA UHITAJI WA KUPUNGUZA BAADHI YA WAFUNGWA KWA FAINI

Baada ya kutembelea katika Gereza la mkoa wa Iringa Mbunge wa Vitimaalumu Mkoani hapa alikutana na changamoto ya mlundikano wa wafungwa wengine wakiwa ni wageni raia wa Ethiopian 12 ambao kwa mujibu wa Mkuu wa Gereza hilo walitakiwa kulipiwa kiasi cha shilingi elfu hamsini 50,000/=ili watolewe kwakuwa nimiongoni mwa wafungwa wasiojihusihsa na jambo lolote katika gereza hilo hivyo Mbunge wa vitimaalum Ritta kabati kulipia fedha hizo na siku ya tarehe 18.12.2013 kufanikiwa kutolewa na kurudishwa nchini kwao ikiwa walishutumiwa kwa uhamiaji haram hapa nchini.

Jumapili, 17 Novemba 2013

MBUNGE WA VITIMAALUM MKOANI IRINGA AWATEMBELEA WAFUNGWA WA GEREZA LA MKOA HUU NAKUZUNGUMZA NAO,AWAHIDI KUWALIPIA FAINI MAHABUSU 12 RAIA WA ETHIOPIA ILI KUPUNGUZA MZIGO GEREZANI HAPO

Mbunge huyo katika kutekereza majukum ya kuwatumikia wananchi wa mkoa wa iringa alipa fulsa hiyo siku chache baada ya kutoka katika vikao vya Bunge mjini Dodoma.

Katika ziara hiyo Mh.Ritta alipata nafasi ya kuzungumza na wafungwa wa geraza hilo na kuwatia moyo kwa changamoto wanazozipata katika gereza hilo ambapo alisema kuwa yeye kama mama mwenye uchungu na mtoto anaumia kuona jamii ya watu wengi wakiwa katika mazingira hayo kwani sikila mtu ayeko gerezani alifanya kosa hata kama alifanya kosa kuna watu wapo nje wanatenda uovu zaidi kuliko makosa yaliyofanywa na wale waliofungwa.

Hivyo kattika mazungumzo hayo alitoa fulsa kwa wafungwa na mahabusu kutoa maoni yao katika maoni hayo alipata ombi la baadhi ya wafungwa wenye maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi waalioomba kulipiwa faini ya shilingi laki moja na elfu ishilini ili waweze kutoka pamoja na kukutana na Raia wa kigeni kutoka nchini Ethiopia 12 waliowekwa mahabusu katuka gereza hilo ambao wanahitaji kiasi cha shilingi elfu hamsini  kila mmoja ambapo jumla ni shilingi laki sita ili kupunguza msongamono wa wafungwa waliopo katika gereza hilo kwani hivi sasa gereza hilo lina jumla ya wafungwa na mahabusu zaidi ya 400 ikiwa gereza hilo linaweza kuchukua wafungwa 228 pekee,hii ikiwa ni kwa mujibu wa mkuu wa Geraza hilo.

Kwa kushirikiana na viongozi wa juu serikalini akiwamo waziri wa sheria na waziri wa mambo ya Ndani Dk.Emmanuel Nchimbi na kuahidi kuzitekeleza baadhi ya changamoto zinazo likabili gereza hilo.

Jumatatu, 11 Novemba 2013

MBUNGE Ritta Kabati aendelea Kuisaidia jamii Mkoani Iringa

Mtoto mlemavu Husein Kafuko wa kijiji cha Itagutwa wilaya ya Iringa vijijini apewa msaada wa Baiskeli ya Miguumitatu na mbunge Ritta Kabati
 
 Katibu wa Mbunge